Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo nchini Tanzania yafikia 69
2023-12-07 09:40:15| CRI

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo kaskazini mwa Tanzania imeongezeka na kufikia 69 baada ya waokoaji kupata miili minne kutoka kwenye tope lililosababishwa na maporomoko hayo Jumatano.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mji wa Katesh, Msemaji mkuu wa serikali na mkurugenzi wa Idara ya Habari Mobhare Matinyi amesema, wataalamu wa jiolojia wa Wizara ya Madini na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) wamesema maafa hayo hayakusababishwa na milipuko ya volcano.

Kwa mujibu wa wataalamu hao, miamba kwenye milima ya Hanang ilizidiwa na maji mengi yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha maporomoko ya udongo na tope.