AU yalaani vurugu zinaziendelea nchini Guinea Bissau
2023-12-07 09:42:08| CRI

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat jana amelaani vurugu zilizofanywa na wafuasi wa kikosi cha ulinzi wa kitaifa nchini Guinea Bissau.

Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika inasema kuwa, Bw. Faki Mahamat ameeleza wasiwasi wake kuhusu kuvunjwa kwa bunge la Guinea Bissau, na kuitaka serikali ya nchi hiyo na pande husika kutoa kipaumbele katika mazungumzo ya amani, na kuheshima katiba, ili kuhakikisha utulivu na muungano wa nchi.

Taarifa hiyo pia imesema, Umoja wa Afrika utaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya hali nchini Guinea Bissau, na kusisitiza kuunga mkono watu na serikali ya nchi hiyo.