Rais Xi Jinping atoa salamu za pole kwa Rais Samia Suluhu kufuatia maporomoko yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini Tanzania
2023-12-08 21:19:50| cri

Rais Xi Jinping wa China jana tarehe 7 Desemba alitoa salamu za pole kwa mwenzake wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kufuatia maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa mkoani Manyara kaskazini mwa Tanzania.

Kwenye salamu zake Rais Xi amesema baada ya kusikia habari kuhusu kutokea kwa maafa hayo na kusababisha vifo, majeruhi na hasara ya mali, kwa niaba ya serikali ya China pamoja na watu wa China, ametoa salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu vilivyosababishwa na janga hilo, na kutoa salamu za pole kwa ndugu waliofiwa na wahanga wa balaa hilo.

Rais Xi ameongeza kuwa anaamini kwamba watu wa Tanzania watashinda maafa hayo na kujenga upya maskani yao.