Baraza la utawala la Sudan lasema limedhamiria kuwezesha kazi za wafanyakazi wa kibinadamu
2023-12-08 10:58:26| cri

Baraza la Utawala wa Mpito la Sudan limesisitiza ahadi yake ya kuwezesha kazi wa wafanyakazi wa kibinadamu na kuondoa vikwazo husika kwa kazi zao.

Taarifa iliyotolewa na Baraza hilo jana imesema, ahadi hiyo ilitolewa katika kongamano kuhusu mwitikio wa kibinadamu lililoitishwa na Kamati ya Pamoja ya Kitaifa kwa Masuala ya Dharura ya Kibinadamu mjini Port Sudan, mji mkuu wa mkoa wa Red Sea.

Makamu mwenyekiti wa Kamati hiyo, Suleiman Al-Dabailo amesema, nchi yake imeweka umuhimu mkubwa katika kuwezesha kazi za wafanyakazi wa kibinadamu. Amesema idadi kubwa ya raia waliokimbia makazi yao tangu mapigano yalipoibuka mwezi April mwaka huu imeweka shinikizo kubwa kwa huduma za afya, elimu, na huduma nyingine za kijamii vijijini na mijini, na kusisitiza haja ya kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia walengwa.