China kufanya kila iwezalo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi duniani
2023-12-08 10:15:15| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Wang Wenbin, amesema kuwa China itaendelea kuhimiza kwa dhati maendeleo ya kijani na endelevu na kufanya kadiri iwezavyo kuchangia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi duniani.

Akiongea na wanahabari Wang Wenbin amesema kuwa China inatilia maanani sana maendeleo ya nishati mbadala. Katika kipindi kifupi, imebadilika kutoka mfuasi na kuwa kiongozi katika nishati mbadala, na uwezo wake uliowekwa, kiwango cha uzalishaji wa nishati, na uwezo wake wa ushindani umeendelea kufikia kiwango kipya. Bw. Wang ameongeza kuwa China inahimiza kikamilifu "kutoa" nishati ya kijani na kusaidia nchi nyingi zinazoendelea kuchora "picha ya kijani".

Hivi karibuni, nchi zaidi ya 100 zilikubaliana katika Mkutano wa 28 wa Nchi watia saini wa Mkataba wa Mfumo wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa (COP28) kuongeza mara tatu uwezo uliowekwa wa kimataifa wa kuzalisha nishati mbadala ifikapo mwaka 2030. Baadhi ya vyombo vya habari vya kigeni vinadai kuwa China ndiyo nchi pekee kubwa inayotarajiwa kufikia lengo hili.