Jeshi la Somalia lawaua wapiganaji 33 wa kundi la al-Shabaab
2023-12-08 22:56:42| cri

Jeshi la Somalia limewaua wapiganaji 33 wa kundi la al-Shabaab na kuwajeruhi wengine kadhaa katika operesheni maalum iliyofanyika karibu na mji wa Haradhere katikati ya Somalia.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Utalii nchini Somalia, Yusuf Al-Adala amesema, jeshi hilo lililenga kambi muhimu ya kundi la al-Shabaab, na kuharibu kituo cha kamandi cha kundi hilo na kukamata shehena kubwa ya silaha.

Ameongeza kuwa, serikali imedhamiria kudumisha operesheni dhidi ya wapiganaji wa kundi la al-Shabaab katika mkoa wa Kati nchini Somalia ili kuhakikisha usalama unadumu nchini humo.

Kundi la al-Shabaab halijatoa kauli yoyote kuhusu operesheni za hivi karibuni katika mkoa wa Galmudug nchini Somalia.