Meli ya Ufilipino yagonga kwa makusudio meli ya ulinzi wa pwani ya China
2023-12-10 11:54:24| CRI

Meli tatu za Ufilipino zikiwemo meli mbili za kikosi cha walinzi wa pwani, moja ya kikazi na moja ya utoaji wa huduma Jumapili ziliingia katika eneo la bahari karibu na Ren’ai Jiao, visiwa vya Nansha, China, bila ya idhini ya serikali ya China, ambapo walinzi wa pwani wa China walichukua hatua za udhibiti dhidi ya meli hizo kwa kufuata sheria.

Meli moja ya Ufilipino ilikaidi maonyo rasmi ya upande wa China, na kwenda kinyume na kanuni za kimataifa za kuepuka meli kugongana baharini, na kubadili njia kwa ghafla bila ya utaalam na kugonga kwa makusudio meli ya ulinzi wa pwani ya China iliyokuwa ikitekeleza sheria.