Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan yawataja wanadiplomasia 15 wa UAE kuwa "watu wasiokaribishwa"
2023-12-11 10:39:47| cri

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imewataja wanadiplomasia 15 kutoka Ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) nchini Sudan kama "watu wasiokaribishwa" na kuwataka waondoke ndani ya saa 48. Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan ilimwita Badria Shehi, kaimu balozi wa Ubalozi wa UAE nchini Sudan na kumfahamisha kuhusu uamuzi huo.

Mapigano kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) yalizuka huko Khartoum tarehe 15 mwezi Aprili, na kisha kuenea katika maeneo mengine ya Sudan na yameendelea hadi leo. Mwishoni mwa Novemba, ofisa wa serikali ya Sudan aliishutumu serikali ya UAE kuunga mkono kikosi cha RSF, na kusababisha mvutano kati ya nchi hizo mbili.