Kipindi cha Hadithi za Jadi Anazopenda Xi Jinping toleo la pili (season 2) kwa lugha ya Kivietnam chaanza kuoneshwa
2023-12-11 19:20:00| cri

Kabla ya katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC na rais wa China Xi Jinping kufanya ziara nchini Vietnam, kipindi cha Hadithi za Jadi Anazopenda Xi Jinping toleo la pili (season 2) kwa lugha ya Kivietnam kimeanza kuoneshwa siku ya Jumatatu nchini Vietnam.

Kipindi cha Hadithi za Jadi Anazopenda Xi Jinping kimechagua misemo mbalimbali ya jadi aliyonukuu rais Xi Jinping kwenye hotuba na makala zake, ikionyesha sifa ya kipekee ya utamaduni wa Kichina, pamoja na maana kuu ya zama za leo na utandawazi.