Rais wa China ahutubia Mkutano wa Kamati Kuu ya CPC na wawakilishi wasio wa CPC
2023-12-11 10:57:54| cri

Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imefanya mkutano na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya kidemokrasia nchini, Shirikisho la Viwanda na Biashara la China na watu wasio na vyama, ili kusikiliza maoni na mapendekezo kuhusu hali ya uchumi ya mwaka huu, na kazi ya uchumi ya mwaka kesho.

Akihutubia mkutano huo uliofanyika mjini Beijing, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni rais wa China, Xi Jinping, amesema, mwaka ujao utakuwa ni Maadhimisho ya Miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, vilevile ni mwaka muhimu wa utekelezaji wa Mpango wa 14 wa Miaka Mitano. Amesisitiza kuwa inapaswa kufuata itikadi ya Ujamaa wenye umaalumu wa China katika kipindi kipya, kuhimiza ukuaji wa uchumi kwa njia yenye ufanisi, kuboresha maisha ya watu, na kudumisha utulivu wa jamii, ili kusukuma mbele kwa pande zote ujenzi wa nchi yenye nguvu zaidi na ustawi wa taifa kwa njia ya kisasa yenye umaalumu wa China.