Maelfu ya watu wakimbia vurugu zinazoendelea mashariki mwa DRC
2023-12-11 08:58:46| CRI

Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imeeleza wasiwasi juu ya kuongezeka kwa vurugu katika sehemu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambazo zimesababisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao kwenye eneo la Masisi, mkoa wa Kivu Kaskazini nchini humo.

OCHA imesema moja ya vijiji vilivyoathirika na vurugu hizo ni Bihambwe, ambacho maelfu ya wanaume, wanawake na watoto walitafuta hifadhi kutokana na vurugu za awali.

Ofisi hiyo imesema wafanyakazi wa mashirika ya kibinadamu wanakumbwa na vizuizi vikubwa katika kutoa misaada kwenye eneo hilo, na kwamba barabara inayounganisha Goma na katikati ya mji wa Masisi imefungwa.