IGAD yafanya mkutano maalum kuhusu suala la Sudan
2023-12-11 08:59:28| cri

Shirika la Maendeleo la Serikali za Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) limefanya mkutano maalum kuhusu suala la Sudan huko Djibouti ambao ulihudhuriwa na viongozi wa nchi wanachama wa Shirika hilo wakiwemo kutoka Sudan, Djibouti, Kenya, Somalia, Ethiopia, Sudan Kusini, na Uganda .

Katika hotuba zao, viongozi wengi walisisitiza umuhimu wa kumaliza vita na kudumisha usalama na utulivu nchini Sudan na katika kanda hiyo.

Katika hotuba yake, mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Mpito nchini Sudan na Kamanda wa Jeshi la nchi hiyo, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan alisisitiza azma ya serikali na jeshi la Sudan kutafuta suluhisho la kina la mgogoro wa nchini humo, kumaliza vita na kufikia amani, na kukaribisha juhudi zote zinazolenga suluhisho la amani la mgogoro wa Sudan. Jenerali al-Burhan pia amesema Sudan lazima ilinde kwa uthabiti mamlaka yake, uhuru na ukamilifu wa ardhi, na kukataa nguvu zote za nje zinazoingilia masuala ya ndani ya Sudan.