Mvua ya nusu saa yakosesha makazi watu 300 Kilosa, Morogoro
2023-12-11 10:38:53| cri

Zaidi ya wananchi 300 wamekosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kubomoka na nyingine kuingiliwa na maji wilayani Kilosa Mkoani Morogoro kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia Desemba 10.

Mvua hiyo iliyonyesha kwa muda wa nusu saa, pamoja na kusababisha athari kwa makazi ya watu, pia imeathiri madaraja manne yakiwemo madaraja ya muda ya Mazinyungu na Wailonga, yanayounganisha mji wa Kilosa, Dumila na maeneo mengine. Madhara mengine ni kumeguka kwa sehemu ya maungio ya daraja la Mto Mkondoa, panapoungana reli, daraja na barabara ambazo zimemeguka sehemu kubwa na kufanya barabara ya kutoka Kilosa kwenda Mikumi na maeneo mengine ya ukanda huo kushindwa kupitika kwa magari.