Wakenya waliosoma nchini China washerehekea miaka 60 ya urafiki kati ya China na Kenya
2023-12-11 09:00:05| CRI

Wanachama wa Shirikisho la Wakenya waliosoma nchini China wamesherehekea miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Kenya.

Katika sherehe hizo zilizofanyika jijini Nairobi, mji mkuu wa Kenya, zaidi ya Wakenya 100 waliosoma katika vyuo vikuu nchini China walikutana na kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kung fu ya kichina, muziki wa jadi wa kichina, na mashairi.

Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Henry Rotich amesema, urafiki kati ya Kenya na China ni ushuhuda wa uhusiano mzuri ulioshinda changamoto na kufanikiwa kupitia uratibu, kuheshimiana na maslahi ya pamoja.

Naye Waziri Mshauri wa Ubalozi wa China nchini Kenya, Zhang Zhizhong amesema Wakenya waliosoma nchini China ni daraja la uhusiano mzuri kati ya nchi hizo mbili, na kuongeza kuwa, miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Kenya imekuwa na manufaa kwa pande zote mbili.