Nukuu za vitabu alizotumia Xi Jinping (sehemu ya pili) toleo la kivietnam yatolewa nchini Vietnam
2023-12-11 16:23:36| cri

Wakati rais Xi Jinping wa China akifanya ziara ya taifa nchini Vietnam, “Nukuu za vitabu alizotumia Xi Jinping” (sehemu ya pili) toleo la kivietnam lililotengenezwa na Shirika kuu la utangazaji la China CMG, kuanzia Desemba 11 linarushwa hewani nchini Vietnam.

Katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika huko Hanoi, mkuu wa shirika la CMG Bw. Shen Haixiong, mkuu wa Radio VOV Tien Sy Do wametoa hotuba kwa njia ya video na karatasi, Naibu mkuu wa radio ya VOV Bw. Minh Hien Ng na watu mashuhuri kutoka sekta za vyombo vya habari na sayansi za kijamii za Vietnam pia wamehudhuria hafla hiyo.

“Nukuu za vitabu alizotumia Xi Jinping” imechagua nukuu za vitabu vya kale zilizotumiwa na rais Xi katika hotuba zake, makala na mazungumzo muhimu, ikionesha kidhahiri urithi mkubwa wa kina wa kiutamaduni na moyo wake wa kutoa kipaumbele kwa watu na kujali nchi na dunia.