Watu 14 wafariki katika ajali ya moto kaskazini mwa Iraq
2023-12-11 09:51:22| cri

Watu 14 wamefariki na wengine 18 kujeruhiwa baada ya moto ulizuka katika jengo la bweni la Chuo Kikuu cha Soran, Kaskazini mwa Iraq usiku wa ijumaa iliyopita. 

Taarifa iliyotolewa na Idara ya afya ya mji wa Soran imesema, moto huo umezimwa na idara ya ulinzi wa raia, na uchunguzi wa awali ulibaini kuwa moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme . 

Mamlaka ya huko imesema uchunguzi wa kina kuhusu ajali hiyo unaendelea, na kusema itafanya kila linalowezekana kuhudumia watu walioathiriwa na moto huo.