Rais wa China afanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV)
2023-12-12 21:25:54| CRI

Rais wa China Xi Jinping Jumanne amefanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) Nguyen Phu Trong huko Hanoi, Vietnam.

Katika mazungumzo hayo, Rais Xi amesema China inaunga mkono kithabiti Vietnam kuendelea kuhimiza   mambo ya ujenzi ya kijamaa , na kwamba anaamini kuwa chini ya uongozi wa kamati Kuu ya CPV, chama na serikali ya Vietnam   vitakamilisha kwa mafanikio majukumu yote yaliyowekwa katika Mkutano Mkuu wa 13 wa Chama cha CPV, na kuweka msingi thabiti kwa ajili ya kutimiza malengo ya ujenzi wa chama na wa nchi hiyo.

Rais Xi pia amesisitiza kuwa  angependa kushirikiana na Bw. Nguyen Phu Trong kutangaza   hadhi mpya ya uhusiano kati ya vyama na serikali za China na Vietnam, na kujenga kwa pamoja Jumuiya ya China na Vietnam yenye Mustakabali wa Pamoja ambayo ina umuhimu wa kimkakati.