China yatoa wito kwa jamii ya kimataifa kuepuka kuingilia masuala ya ndani ya DRC
2023-12-12 08:42:29| cri

Naibu mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing ameitaka jamii ya kimataifa kuepuka kuingilia masuala ya ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Balozi Dai amesema hayo jana katika kikao cha Baraza la Usalama kuhusu hali ya DRC, na kusema nchi hiyo iko katika hatua muhimu katika kukuza mchakato wa kisiasa na kudumisha usalama na utulivu. Amesema uchaguzi mkuu nchini DRC utafanyika hivi karibuni, na kuitaka jamii ya kimataifa kuheshimu kikamilifu mamlaka na uongozi wa DRC, kuhimiza pande zote kutatua tofauti kwa njia ya mazungumzo na mashauriano, na kuepuka kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo.