Makamu mkuu wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Fedha za Maendeleo, Akihiko Nishio, aipongeza Tanzania kwa maendeleo katika kupunguza umaskini
2023-12-12 10:58:02| cri

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Fedha za Maendeleo Bw. Akihiko Nishio, amesema Zanzibar na Serikali ya Tanzania zimepata mafanikio muhimu ya kimaendeleo katika miaka kadhaa iliyopita. Amesema kutokana na uungaji mkono wa jumuiya ya maendeleo ya misaada ya benki ya dunia IDA, katika nusu ya kwanza ya mzunguko wa IDA20, watu milioni 6.6 nchini Tanzania walipatiwa fursa ya kuboresha huduma za usafi, na wanafunzi milioni 2.5 walinufaika kutokana na kuboreshwa kwa mazingira ya elimu, na nusu ya wanafunzi hao ni wasichana. Bwana Nishio amesema mafanikio hayo makubwa yanaleta mabadiliko ya kweli katika maisha ya watu.

Amesema mkuu wa benki ya dunia Bw. Ajay Banga ameweka kuleta mabadiliko kwenye maisha ya watu kuwa ni kipaumbele kwa IDA kuwa na mafanikio makubwa.