Mazungumzo kati ya Israel na kundi la Hamas kuhusu kuachiwa kwa wafungwa yatarajiwa kuanza wiki ijayo
2023-12-12 10:55:21| cri

Televisheni ya Al Arabiya leo asubuhi imesema mazungumzo kati ya Israel na Kundi la Hamas kuhusu kuachiwa kwa wafungwa yanatarajiwa kuanza wiki ijayo. Kundi la Hamas lilitoa wito wa kusitisha mapigano kwa pande zote lakini halikukataa kabisa "usitishwaji vita wa kibinadamu chini ya hali mpya."

Kwa mujibu wa ripoti ya chaneli ya kiarabu ya televisheni ya Sky News ya Uingereza tarehe 12, Israel ilizitaka Misri na Qatar kufanya usuluhisho na kufikia makubaliano mapya ya kubadilishana wafungwa.

Kwa upande mwingine, ofisa mwandamizi wa kundi la Hamas Bw. Osama Hamdan alitoa taarifa akisema kuwa serikali ya Israel ililazimishwa na shinikizo la ndani kutoa uvumi juu ya kuanzishwa tena kwa mazungumzo ya kusitisha mapigano, lakini msimamo wa Hamas uko wazi, yaani hakutakuwa na mabadilishano ya wafungwa kabla ya usitishaji kamili wa mapigano katika Ukanda wa Gaza.