Ripoti yaonyesha 9% waongezeka kwenye uandikishaji wa bima ya afya ya jamii nchini Uganda
2023-12-12 10:57:35| cri

Ripoti mpya iliyotolewa na Ofisi ya Matibabu ya Kiprotestanti Uganda (UPMB) inaonyesha kuwa watu wengi zaidi wanajiandikisha katika mipango ya bima ya afya ya jamii. Ripoti hiyo inaonesha kuwa kati ya Julai 2022 na Juni 2023 pekee, katika programu mbili za bima chini ya UPMB, kulikuwa na ongezeko la asilimia 8.9 la wanachama kutoka 94,047 hadi 102,461.

Akizungumza kwenye mahojiano wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utendaji ya Ofisi ya Matibabu ya Kiprotestanti Uganda ya Julai 2022 - Juni 2023, mkuu wa Ofisi ya uimarishaji wa mifumo ya afya na usimamizi wa wanachama wa ofisi hiyo Dk Hillary Alima, amesema watu wengi wameanza kuona umuhimu wa bima ya afya.