Katibu mkuu wa UM asema mazungumzo ya tabianchi bado yanahitaji “kuondoa pengo kubwa”
2023-12-12 23:24:49| cri

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres tarehe 11 Desemba alipozungumza na wanahabari kando ya mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, alisema kabla ya kufungwa kwa mkutano huo kuwa pengo kubwa bado linahitaji kushughulikiwa, pande zote zinapaswa kufuatilia tabianchi na usawa, na nchi zilizoendelea zinapaswa kutekeleza ahadi zote.

Bw. Guterres amezihimiza nchi zote wanachama ziwe na nia thabiti ya kupunguza utoaji wa hewa ukaa na kutimiza haki ya tabianchi. Pia amezihimiza nchi zilizoendelea zitekeleze ahadi zote vya kutosha na kwa uwazi kuhusu mambo ya fedha na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.