Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Iran wafanya mazungumzo kwa njia ya simu
2023-12-12 14:27:09| cri

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Iran Hossein Amir-Abdollahian, na kubadilishana naye maoni kuhusu hali ya Gaza.

Bw. Amir-Abdollahian amepongeza juhudi za China kuwezesha usimamishaji vita kwa sababu ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza wakati China ilipokuwa mwenyekiti wa zamu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Pia ameishukuru China kwa mchango wake  kwa ajili ya kuhimiza maafikiano kati ya Iran na Saudi Arabia, na kusema Iran  ingependa kuimarisha ushirikiano na China katika nyanja mbalimbali na kuhimiza   uhusiano kati ya China na Iran uendelezwe siku hadi siku .

Kwa upande wake Wang Yi amesema China ingependa kushirikiana na Iran katika kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa kati ya Rais Xi Jinping na Rais Ebrahim Raisi kwenye mkutano wao mwaka huu.

Amesema China  itaongeza mawasiliano,  kuimarisha hali ya kuaminiana, kupanua ushirikiano,  kufanya uratibu na kushirikiana na Iran katika mambo  ya kimataifa na ya pande nyingi,  kufanya ushirikiano wa pande nyingi ulio wa kweli, kulinda haki na maslahi halali ya nchi hizo mbili na ya nchi zinazoendelea,  na kulinda haki na usawa  katika mambo ya kimataifa, kusukumba mbele maendeleo tulivu na endelevu ya uhusiano wa China na Iran.

Amesema China inaziunga mkono Iran na Saudi Arabia kuendelea kuboresha uhusiano, kuhimiza  mshikamano na ushirikiano kati ya nchi za kikanda, na  kujiamulia zenyewe amani na usalama wa kikanda.