Mkutano wa kazi ya uchumi ya Kamati Kuu ya CPC wafanyika mjini Beijing
2023-12-12 21:24:41| CRI

Mkutano wa kazi ya uchumi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umefanyika mjini Beijing ambapo Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni Rais wa China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi Xi Jinping amehudhuria na kutoa hotuba muhimu.

Katika hotuba yake Rais Xi  amefanya majumuisho kwa pande zote kazi ya uchumi ya mwaka 2023, kuchambua kwa kina hali ya hivi sasa ya kiuchumi, na kuweka majukumu ya uchumi ya mwaka 2024.

Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni Waziri Mkuu wa China Li Qiang alitoa hotuba  akifanya majumuisho ya kazi na kutoa matakwa ya   kutekeleza maagizo aliyotoa Rais Xi katika hotuba yake na majukumu ya uchumi ya mwaka ujao.