China yasifiwa kwa kutoa mchango mkubwa katika kulinda usalama wa chakula duniani
2023-12-12 08:43:42| cri

Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kongo (Kongo Brazzaville) Mamadou Mbaye, amesema, msaada wa chakula unaotolewa na serikali ya China barani Afrika umetoa mchango mkubwa katika kulinda usalama wa chakula barani humo na duniani.

Akizungumza katika hafla ya kusaini hati ya kukamilika kwa mradi wa China kutoa msaada wa chakula hapo jana akiwa pamoja na Balozi wa China nchini Jamhuri ya Kongo Bw. Li Yan, Bw. Mbaye amesema, China imekuwa mstari wa mbele kuzisaidia nchi za Afrika zinapokabiliwa na matatizo. Amesema China na mashirika ya Umoja wa Mataifa zimetekeleza miradi mingi ya ushirikiano barani Afrika, na kutoa mchango mkubwa kwa kulinda usalama wa chakula wa nchi za Afrika ikiwemo Jamhuri ya Kongo.