Hujambo, Vietnam!
2023-12-12 14:14:26| cri

Kutokana na mwaliko wa katibu mkuu wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisiti cha Vietnam CPV Nguyen Phu Trong na rais wa Vietnam Vo Van Thuong, rais Xi Jinping wa China Desemba 12 na 13 atafanya ziara nchini Vietnam.

Vietnam iko mashariki mwa peninsula ya Katika na Kusini, ikiwa na eneo la kilomita laki 3.3 za mraba. China na Vietnam ni nchi majirani kijiografia, ambazo pia ni wenzi muhimu wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara. China siku zote ni mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Vietnam, huku Vietnam ikiwa mwenzi mkubwa zaidi wa China katika ASEAN mwenzi mkubwa wa nne wa kibiashara wa China duniani.

Huu ni mwaka wa maadhimisho ya miaka 15 tangu China na Vietnam zianzishe uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote. China na Vietnam ni majirani wazuri, marafiki wakubwa na ndugu wa chanda na pete.