Mkutano wa 12 wa nishati wa nchi za kiarabu wafunguliwa mjini Doha, Qatar
2023-12-12 10:24:13| cri

Mkutano wa 12 wa nishati wa nchi za kiarabu ulifunguliwa jana mjini Doha, Qatar. Maafisa wa ngazi ya uwaziri kutoka Qatar, Iraq, Kuwait, Algeria, Libya wamehudhuria mkutano huo na kujadili mada mbalimbali zikiwemo usalama wa nishati, uhifadhi wa mazingira, maendeleo endelevu n.k.

Waziri wa nishati wa Qatar Bw. Saad al-Kaabi amesema kwenye mkutano huo kuwa nchi mbalimbali duniani zinatakiwa kuimarisha ushirikiano, kuongeza uwekezaji katika teknolojia ya kupunguza utoaji wa hewa ukaa na kuhimiza maendeleo ya nishati endelevu.