Wataalamu wa China wafanya ukaguzi wa reli ya TAZARA
2023-12-13 08:42:00| CRI

Kampuni ya Ujenzi na Uhandisi ya China (CCECC) imepeleka kikosi kazi cha wataalamu kufanya ukaguzi wa kina wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).

Katika taarifa yake iliyotolewa jana na TAZARA, ukaguzi huo utafanyika kuanzia Dar es Salaam nchini Tanzania hadi New Kapiri Mposhi nchini Zambia, na unalenga kutathmini utendaji kazi wa reli hiyo na mfumo wa biashara, na kuwasilisha kwa wadau wa reli hiyo, muswada wa Kampuni hiyo wa kunufaika zaidi na matumizi ya reli hiyo.

Mwezi Agosti mwaka jana, rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na mwenzake wa Zambia, Hakainde Hichilema walikubaliana kukusanya rasilimali ili kufufua reli ya TAZARA na kuifanya kuwa na kisasa zaidi.

Reli ya TAZARA ilijengwa kati ya mwaka 1970 na 1975, kupitia mkopo usio na riba kutoka China, na ilianza rasmi kufanya kazi mwezi Julai mwaka 1976.