Ushirikiano kati ya China na Afrika waongeza msukumo kwa maendeleo ya uchumi wa kidijitali barani Afrika
2023-12-13 08:41:09| cri

Naibu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Biashara Duniani Bw. Zhang Xiangchen amesema, katika miaka ya hivi karibuni, licha ya kufufuka polepole kwa uchumi wa dunia, nchi nyingi zaidi za Afrika zimetumia uchumi wa kidijitali kama injini mpya ya kukuza maendeleo.

Akizungumza jijini Nairobi, Kenya, hivi karibuni, Bw. Zhang amesema China na Afrika ni wenzi wa ushirikiano katika mchakato wa Afrika wa kuendeleza uchumi wa kidijitali na kufikia malengo yake ya kisasa.

Pia amesema, pande hizo mbili zimedumisha uhusiano wa karibu kwa muda mrefu, na uzoefu wa maendeleo wa China una thamani muhimu kwa Afrika, na kuongeza kuwa, katika siku zijazo, makampuni mengi zaidi ya China yataongeza uwekezaji barani Afrika na kukuza mageuzi ya kidijitali barani humo.