ADB yaongeza makadirio ya ukuaji wa uchumi wa China kwa mwaka 2023 hadi asilimia 5.2
2023-12-14 08:52:31| cri

Ripoti ya "Makadirio ya Maendeleo ya Asia 2023 (Toleo la Desemba)" iliyotolewa jana na Benki ya Maendeleo ya Asia imekadiria kuwa kiwango cha ukuaji wa uchumi wa China cha mwaka huu kitafikia asilimia 5.2, ikiwa ni zaidi ya kiwango cha asilimia 4.9 kilichotolewa mwezi Septemba.

Ripoti hiyo imesema uchumi wa China umedumisha kasi ya ukuaji katika robo ya tatu ya mwaka, ikichochewa na mambo kadhaa ikiwemo kuongezeka kwa matumizi ya kaya na uwekezaji wa umma.

Ripoti hiyo pia imekadiria kuwa, uchumi unaoendelea katika eneo la Asia-Pasifiki utakua kwa asilimia 4.9 mwaka huu, ikiwa ni asilimia 0.2 zaidi ya makadirio ya mwezi Septemba, na utakua kwa asilimia 4.8 mwaka 2024, sawa na makadirio ya awali.