Kiongozi wa ujumbe wa China katika mkutano wa COP28 amesema juhudi za China zimetia msukumo mkubwa wa kisiasa katika kufanikisha mkutano huo
2023-12-14 22:45:12| cri

Kiongozi wa ujumbe wa China katika Mkutano wa 28 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) Bw. Zhao Yingmin jana tarehe 13 alipozungumzana na mwandishi wa habari wa Shirika Kuu la Utangazaji la China, amesema China inatilia maanani mkutano huo ambao ni muhimu katika mchakato wa usimamizi wa tabianchi duniani ambapo ilitia msukumo mkubwa wa kisiasa ili kuufanikisha.

Bw. Zhao amesema matokeo mengi yaliyopatikana katika mkutano huo yameonyesha juhudi za kimataifa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, huku yakilingana na dhana ya ustaarabu wa ikolojia na kukuza mabadiliko ya kijani iliyopendekezwa na China. Amesema China inaamini kuwa mkutano huu kimsingi umekidhi matarajio na umeelekeza hatua zifuatazo za usimamizi wa tabianchi duniani.