Watu milioni 4 walioathirika na mafuriko Afrika Mashariki wanahitaji msaada wa kibinadamu
2023-12-14 14:07:17| cri



Shirika la hisani la kimataifa Oxfam hivi karibuni limeonya kuwa, zaidi ya watu milioni 4 walioathiriwa na makubwa yalikumba sehemu kubwa ya mashamba katika Afrika Mashariki wanahitaji sana msaada wa kibinadamu. 

Oxfam ilisema mvua kubwa zilizoanza mwezi Oktoba, zimesababisha vifo vya mamia ya watu, kusomba maelfu ya nyumba na kuharibu mazao ya wakulima nchini Kenya, Ethiopia, na Somalia yaliyokuwa kwenye kipindi cha katikati cha msimu wa mavuno. 

Mkurugenzi wa Oxfam kanda ya Afrika Fati N'zi-Hassane amesema hali mbaya ya hewa ni changamoto kubwa kwa watu wanaokabiliwa na njaa na umaskini katika eneo la Afrika Mashariki.