Ukuaji wa uchumi wa nchi za Afrika Mashariki huenda ukapungua kwa mwaka 2024
2023-12-14 08:55:04| CRI

Kampuni ya kimataifa ya ukaguzi wa mahesabu Deloitte imesema, nchi za kanda ya Afrika Mashariki zinaweza kukabiliwa na ukuaji mdogo wa uchumi katika mwaka 2024 baada ya kukabiliana na changamoto zilizojitokeza mwaka huu.

Katika ripoti yake iliyotolewa jana jijini Nairobi, Kenya, kampuni hiyo imetoa makadirio ya kina ya mtazamo wa uchumi kwa hivi sasa katika kanda hiyo, uliokabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kushuka kwa thamani ya sarafu za nchi hizo, kuongezeka kwa gharama za maisha, ukame, ongezeko la deni la umma na mvutano wa siasa za kijiografia.

Mshauri wa masuala ya uchumi wa Afrika katika kampuni hiyo, Tewodros Sisay amesema, ukuaji wa uchumi wa Afrika Mashariki unatarajia kurejea tena mwaka 2024, na kuongezeka kwa kiwango cha asilimia 6.5. Amesema ongezeko hilo litatokana na kufufuka kwa kikamilifu kwa sekta ya huduma, kuboreshwa kwa biashara ya nje na kufufuka kwa matumizi binafsi.