WFP yatoa wito kwa pande hasimu za Sudan zisimamishe vita
2023-12-14 23:11:38| cri

Shirika la Mpango wa Chukua Duniani (WFP) limetoa wito kwa pande mbili zinazopambana nchini Sudan zisimamishe vita mara moja kwa sababu za kibinadamu, na kuruhusu msaada wa kibinadamu uingie bila vizuizi, ili kuepuka baa kubwa la njaa nchini Sudan.

WFP imesema kwa sasa watu takriban milioni 18 wa Sudan wanakumbwa na hali mbaya ya ukosefu wa chakula, idadi ambayo inazidi kwa mara mbili ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huo, na watu takriban milioni 5 kati yao wako katika hali ya dharura ya chakula. Shirika hilo limeonya kuwa hadi kufikia mwezi Mei mwakani wakati msimu wa kiangazi utakapoingia nchini humo, kama hakuna ongezeko kubwa la msaada wa chakula, baadhi ya sehemu za Sudan zinaweza kukumbwa na baa kubwa la njaa.