Marekani na eneo la Caribbean zaripoti wagonjwa zaidi milioni 4 walioambukizwa homa ya dengue mwaka huu
2023-12-14 10:15:18| cri

Mwakilishi wa Shirika la Afya la Pan American amesema ongezeko la joto kutokana na mabadiliko ya tabia nchi limesababisha ongezeko la mbu, na kusababisha kuenea kwa homa ya dengue katika eneo la magharibi la dunia. Hadi kufikia mwaka huu, wagonjwa zaidi milioni 4 wa homa ya dengue wameripotiwa nchini Marekani na katika eneo la Caribbean, na kusababisha vifo zaidi ya 2,000.

Wataalamu kutoka Shirika la Afya la Pan American wamesema kuendelea kuongezeka kwa joto kwa mwaka huu kumesababisha ongezeko la mbu, na ukame na mafuriko yanayohusiana na mabadiliko ya tabia nchi yanaongeza kasi ya kuenea kwa virusi. Zaidi ya hayo, hali mbaya ya usafi wa mazingira na mifumo dhaifu ya matibabu katika nchi nyingi za eneo hilo, pia vimechangia ongezeko la maambukizi ya homa ya dengue.