AfDB yaidhinisha dola za kimarekani milioni 5.4 kwa ajili ya Nishati ya Afrika Mashariki
2023-12-15 09:50:50| cri

Ofisa mkuu mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Umeme Uganda Bibi Ziria Tibalwa Waako, amesema Bodi Huru ya Udhibiti (IRB) imepokea dola milioni 5.4 (Sh 20b) kutoka kwa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa ajili ya uendeshaji wa pamoja wa usimamizi wa umeme katika eneo la Afrika Mashariki ( EAPP), kwa lengo la kutoa umeme wa uhakika na wa bei nafuu katika kanda hiyo.

Bibi Waako amesema wadau wa usimamizi wa umeme wa Afrika Mashariki walikaa na kujadili namna ya kuhakikisha kanda hiyo inanufaika na raslimali za nishati mbadala na zenye gharama nafuu ili kuchochea uchumi wake.

Bibi Waako ambaye pia ni mwenyekiti wa IRB amesema lengo lao ni kuhakikisha kuwa nchi wanachama zinafikia ajenda mbili kuu za kubadilisha uchumi wao kuwa uchumi wa viwanda ili kuongeza nafasi za ajira na kuendeleza uchumi.