Kenya na China zaadhimisha miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia
2023-12-15 08:36:46| cri

Kenya na China zimeadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia jana Desemba 14.

Mkuu wa Mawaziri ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje ya Kenya, Bw. Musalia Mudavadi amesema, katika miaka 60 iliyopita, uhusiano kati ya Kenya na China umepata maendeleo makubwa, uaminifu wa kisiasa umeongezeka, na uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya pande hizo mbili umeendelea kuimarika.

Amesema ujenzi wa pamoja wa Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na mipango mingine inaunganisha kwa kina mawazo ya China na Ruwaza ya Maendeleo ya Kenya ya mwaka 2030.

Bw. Mudavadi pia amesema Kenya inatarajia kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, kuimarisha mawasiliano kati ya watu na watu, na kuungana mkono ili kuingia katika miaka mingine 60 mipya.