Rais wa China atuma barua ya pongezi kwa maadhimisho ya miaka 50 ya kamati ya taifa ya biashara ya Marekani na China
2023-12-15 14:24:19| cri

Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa maadhimisho ya miaka 50 ya kamati ya taifa ya biashara ya Marekani na China, akipongeza kamati na wajumbe wake wote na kutoa salamu za dhati kwa watu wa jamii mbalimbali za Marekani wanaofuatilia na kuunga mkono ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani.

Amesema wakati dunia ikikabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayajashuhudiwa katika miaka mia moja iliyopita, China na Marekani kushikana mikono na kushirikiana katika kukabiliana na changamoto kwa pamoja au la kunahusiana na maslahi za nchi mbili na kuathiri hatma ya binadamu wote. Kabla ya hapo, alikutana na mwenzake wa Marekani Joe Biden huko San Francisco, na kubadilishana naye maoni kuhusu masuala makubwa ya uhusiano kati ya China na Marekani na kufikia makubaliano muhimu. Amesema China inapenda kushikilia kanuni za kuheshimiana, kuishi kwa amani, ushirikiano wa kunufaishana, na kufanya juhudi pamoja na Marekani kutekeleza makubaliano ya San Francisco, ili kuhimiza maendeleo yaliyo chanya, endelevu na tulivu ya uhusiano kati ya China na Marekani.

Wakati huohuo, rais Joe Biden wa Marekani pia ametuma barua ya pongezi kwa sherehe ya maadhimisho ya miaka 50 ya kamati ya taifa ya biashara ya Marekani na China.