UN yahofia makabiliano kati ya DRC na Rwanda
2023-12-15 09:51:25| cri

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa (UN) Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Bintou Keita ameeleza wasiwasi kuhusu hatari inayoweza kutokea kutokana na mvutano unaoendelea kati ya DRC na Rwanda.

Bwana Keita Katika wiki za hivi karibuni, hali katika Jimbo la Kivu Kaskazini nchini DRC kwenye mpaka na Rwanda imekuwa ikizorota, na mivutano kati ya pande hizo mbili imekuwa ikiongezeka na kuleta hatari ya makabiliano ya moja kwa moja ya kijeshi yanayoweza kuiathiri hata Burundi.

Uhusiano kati ya DRC na Rwanda, ambao bado haujatulia tangu vita vya miaka ya 1990 na 2000, umedorora katika miaka miwili iliyopita kutokana na kuibuka tena kwa waasi wa kundi la M23 huko Kivu Kaskazini.

DRC inaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono wapiganaji wa kundi hilo wanaoongozwa na Watutsi, ambao wanashikilia eneo kubwa Mashariki mwa nchi hiyo tangu kuanza mashambulizi mwishoni mwa mwaka 2021.