Rais Xi Jinping wa China afanya ziara ya ukaguzi mjini Laibin mkoani Guangxi
2023-12-15 14:23:40| cri

Rais Xi Jinping wa China jana mchana alifanya ziara ya ukaguzi mjini Laibin mkoani Guangxi. Ametembelea bustani ya kilimo cha kisasa ya taifa ya mji wa Laibin, kituo cha miwa bora ya kutengeneza sukari cha Huang’an na kampuni ya sukari ya Fenghuang ya kundi la Dongtang, ili kufahamu kuhusu hali ya uzalishaji wa mbegu za miwa, upandaji na uvunaji wa miwa na maendeleo ya sekta ya sukari.