Marais wa China na Kenya wapongezana kwa kutimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili
2023-12-15 08:36:00| criRais Xi Jinping wa China na rais wa Kenya William Ruto jana wamepeana salamu za pongezi kwa kutimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Rais Xi amesema, tangu China na Kenya zilipoanzisha uhusiano wa kidiplomasia miaka 60 iliyopita, nchi hizo mbili siku zote zimeshirikiana na kupata maendeleo, zimekuwa marafiki wa kuaminiana kisiasa na wenzi wazuri wa ushirikiano wa kiuchumi.

Rais Ruto amesema, Kenya inapenda kushirikiana na China kutimiza matokeo ya Mkutano wa Tatu wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja na Njia Moja uliofanyika mjini Beijing, mazungumzo kati ya viongozi wa China na Afrika uliofanyika huko Johannesburg, Afrika Kusini, ili kuufanya uhusiano kati ya nchi hizo mbili upate maendeleo ya kudumu.