China yatoa magari kwa Uganda kuisaidia kuandaa mkutano wa nchi zisizofugamana na upande wowote
2023-12-15 22:50:00| cri

China imeahidi kuisaidia Uganda wakati ikijiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) na Mkutano wa 3 wa wakuu wa nchi za Kusini.

Balozi wa China nchini Uganda Bw. Zhang Lizhong amesema hayo wakati alipokabidhi magari 70 kwa serikali ya Uganda. Balozi Zhang amesema China itaendelea kuiunga mkono Uganda katika kutekeleza jukumu lake kubwa katika masuala ya kikanda na kimataifa na kuimarisha mshikamano kati ya nchi zinazoendelea kupitia mikutano hiyo.

China imetoa magari hayo 70 kwa ajili ya mikutano ijayo iliyopangwa kufanyika Januari 2024.

Balozi ameitaka mikutano hiyo kuwa itakuwa ni tukio kubwa kwa nchi zinazoendelea kuimarisha mshikamano na kufikia maendeleo pamoja, na kuwa itaongeza zaidi ushawishi wa Uganda katika masuala ya kimataifa.