Rais Xi Jinping wa China afanya ziara ya ukaguzi mjini Nanning, mkoani Guangxi
2023-12-15 10:19:24| cri

Rais Xi Jinping wa China amefanya ziara ya ukaguzi mjini Nanning mkoani Guangxi. Rais ametembelea kampuni ya huduma za taarifa ya China na ASEAN (China-ASEAN information harbor, CAIH) na eneo la makazi la Panlong lililoko wilaya ya Liangqing, na kukagua ujenzi na matumizi ya Tehama na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na ASEAN, kukamilisha mfumo wa usimamizi wa makazi na kuimarisha kazi ya mshikamano wa makabila.