Ndege yaanguka Lamu muda mfupi baada ya kuwashusha wanafunzii bora wa KCPE
2023-12-18 22:58:50| cri

Watu kumi, wakiwemo maafisa saba wa kijeshi, afisa wa polisi, rubani mkuu na rubani mwenzake, walinusurika kufa na kujeruhiwa Jumapili saa saba na nusu mchana wakati ndege ndogo aina ya Cessna ilipoanguka na kuwaka moto baada ya kugonga nguzo ya umeme na waya huko Kiunga, Kaunti ya Lamu kwenye mpaka wa Kenya na Somalia. Nyumba moja iliteketea katika ajali hiyo.

Naibu Kamishna wa Kaunti ya Lamu Mashariki George Kubai alithibitisha ajali hiyo, akisema watu hao kumi walikuwa wakirejea Nairobi baada ya kuwashusha wanafunzi waliofanya vyema katika mtihani wa KCPE wa 2023 ambao walikuwa wanatoka ziara ya kielimu jijini Nairobi. Safari hiyo ilifadhiliwa na mbunge wa eneo hilo.