Chad yawafukuza wanadiplomasia wanne wa Sudan
2023-12-18 09:01:00| CRI

Chad imetangaza kuwa wanadiplomasia wanne wa Sudan ni watu wasiokaribishwa na wanatakiwa kuondoka nchini humo ndani ya masaa 72.

Wizara ya mambo ya nje ya Chad jumamosi ilisema katika taarifa yake kuwa imefanya uamuzi huo kutokana na kauli nzito na isiyo na msingi aliyotoa naibu mkuu wa jeshi la Sudan Luteni Jenerali Yasir al-Atta akiituhumu Chad kuingilia kati mgogoro wa ndani wa Sudan. Chad ilimwita balozi wa Sudan nchini humo na kumfahamisha kuhusu uamuzi huo.

Taarifa hiyo pia imeongeza kuwa kutoa maoni kama hayo tena kwa mamlaka ya Sudan dhidi ya Jamhuri ya Chad na serikali yake ni jambo lisilokubalika, lisilo la kirafiki na linaonyesha nia ovu.