Rais Xi atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Emir wa Kuwait Sheikh Nawaf
2023-12-18 08:20:08| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za rambirambi kwa Emir mpya wa Kuwait Sheikh Mishal Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah kufuatia kifo cha Emir Sheikh Nawaf Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah.

Kwa niaba ya serikali ya China na wananchi wake na yeye mwenyewe, Rais Xi ametoa salamu za rambirambi kwa familia ya  Sheikh Nawaf na watu wa Kuwait kutokana na kifo chake.

Rais Xi amesema Sheikh Nawaf aliheshimiwa na kupendwa na watu wa Kuwait na alitoa michango chanya kwenye maendeleo ya uhusiano kati ya China na Kuwait.

Mjumbe maalumu wa Rais Xi Jinping, Bw. Shohrat Zakir atahudhuria shughuli za maombolezo ya kifo cha Sheikh Nawaf zitakazofanyika leo Desemba 18.