Rwanda yapata dola za kimarekani milioni 268 kutoka IMF ili kukabiliana na athari za hali ya hewa
2023-12-18 14:53:29| cri

Rwanda imepata dola za Kimarekani milioni 268 kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ili kukabiliana na athari za hali ya hewa.

Wizara ya fedha ya Rwanda imesema kuwa fedha hizo zilizoidhinishwa chini ya Mfumo mpya wa Mikopo iliyowekwa tayari, pia zitatumika kuongeza urari wa malipo.

Taarifa ya IMF imesema kuwa dhamira ya Rwanda ya kujenga uchumi imara na wa kijani ni ya kupongezwa na inatakiwa kudumishwa. Imeongeza kuwa kuimarisha mipango ya ulinzi wa kijamii, kuongeza ulimbikizaji wa ujuzi wa watu, na kukuza uchumi anuai unaoongozwa na sekta binafsi itakuwa muhimu katika kukabiliana na nyakati zenye changamoto na kuboresha viwango vya maisha.