Mjumbe maalum wa rais wa China ahudhuria hafla ya kuapishwa kwa rais wa Madagascar
2023-12-18 08:47:57| CRI

Kutokana na mwaliko wa rais Andry Nirina Rajoelina wa Madagascar, Mjumbe maalum wa Rais wa China Bw. Hu Chunhua, ambaye ni naibu mwenyekiti wa kamati ya baraza la mashauriano ya kisiasa la China, amehudhuria hafla ya kuapishwa kwa rais Rajoelina na kukutana na rais huyo.

Bw. Hu amewasilisha salamu za rais Xi, huku akisema China inatilia maanani katika kuendeleza uhusiano na Madagascar na inapenda kushirikiana na nchi hiyo kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali na kuendelea kuungana mkono kwenye masuala yanayohusiana na maslahi kuu na ufuatiliaji mkubwa wa upande mwingine, ili kuhimiza uhusiano wa ushirikiano.

Rais Rajoelina ametoa shukrani kwa mjumbe maalumu wa rais wa China kuhudhuria hafla hiyo, na kusema, Madagascar inazingatia urafiki wa jadi kati yake na China, na kupenda kushirikiana na China katika sekta mbalimbali.