Ujumbe wa Chama cha Kikomunisti cha China watembelea Cote d'Ivoire
2023-12-18 08:59:55| CRI

Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) katika Shirikisho Kuu la Wanawake la China ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa shirikisho hilo Bi. Huang Xiaowei, ameongoza ujumbe wa chama hicho kutembelea Cote d'Ivoire kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 17 mwezi huu, na amefanya mazungumzo na naibu spika wa bunge la Cote d'Ivoire na katibu mtendaji wa Chama cha Umoja cha Cote d'Ivoire na kutembelea makazi na vijiji nchini humo akieleza Fikra ya Xi Jinping kuhusu ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya, na kubadilishana nao maoni kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya marais wa nchi hizo mbili na kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya China na Côte d'Ivoire.

Côte d'Ivoire imesema inapenda kutumia vizuri fursa ya maadhimisho ya miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia kati yake na China kuimarisha hali ya kuaminiana kisasa na kuzidisha mawasiliano na ushirikiano katika mambo ya vyama, wanawake, vijana na familia.