Kampuni ya Huawei ya China yawatunuku vyeti wanafunzi wa Tanzania
2023-12-19 09:01:17| CRI

Kampuni ya Tehama ya China Huawei ilifanya sherehe ya kuwatunuku vyeti wanafunzi wa Tanzania walioshiriki kwenye programu yake iitwayo Seeds for the Future (SFTF) mjini Dar es Salaam jana Jumatatu.

Waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari wa Tanzania Bw. Nape Nnauye, alipongeza uungaji mkono wa Huawei katika kuandaa vijana wenye vipaji katika nyanja ya habari, mawasiliano na teknolojia, akisema hii ndio misukumo mikuu kwa mageuzi ya kidijitali na uchumi unaotegemea utaalamu.
Bw. Nnauye alisema hayo wakati aliwapotunuku vyeti wanafunzi wa vyuo vikuu walioshiriki kwenye programu ya SFTF, iliyoanzishwa mwaka 2016 nchini Tanzania kwa lengo la kuhimiza maendeleo ya Tehama na kuchangia utimizwaji wa ruwaza ya uchumi wa kidijitali ya nchi hiyo.